Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China imezitaka Marekani na Korea Kusini ziondoe vifaa hivyo na kusimamisha uwekaji huo. Amesema uwekaji wa mfumo wa THAAD utaharibu uwiano wa kimkakati wa kanda hiyo, kusababisha hali ya Peninsula ya Korea izidi kuwa mbaya, na pia kuharibu vikali maslahi ya usalama wa kimkakati wa China. Ameongeza kuwa China itachukua hatua zote zinazohitajika kulinda maslahi yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |