• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yawapatia chanjo karibu nusu ya watoto duniani

    (GMT+08:00) 2017-04-27 09:18:01

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema mwaka jana lilitoa chanjo bilioni 2.5 kwa watoto katika nchi 100, likiwafika karibu nusu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kote duniani. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Nigeria, Pakistan na Afghanistan ambazo bado zinaathiriwa na ugonjwa wa polio, zimepewa chanjo nyingi zaidi kuliko nchi nyingine duniani. Bw. Dujarric pia amesema bado kuna watoto milioni 19.4 kote duniani wanaokosa chanjo kila mwaka kutokana na mapigano, mfumo dhaifu wa afya, umaskini au ukosefu wa haki kwenye jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako