• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yailaani Marekani kwa kuitisha mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu kuiwekea vikwazo

    (GMT+08:00) 2017-04-27 09:47:54
    Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imeilaani Marekani kwa kutaka kuitisha mkutano wa Baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, kwa lengo la kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

    Amesema kwa upande mmoja Marekani inaitaja Korea Kaskazini kuwa ni tishio, kwa upande mwingine imeweka silaha za nyuklia kwenye peninsula la Korea na kufanya mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi na Korea Kusini na kuiweka kanda hiyo kwenye hatari ya kutokea kwa vita vya nyuklia.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na waziri wa ulinzi na mkurugenzi wa ujasusi wa Marekani inasema, rais Donald Trump anataka kuilazimisha Korea Kaskazini iache mpango wa kuendeleza silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu kwa kuiwekea zaidi vikwazo vya kiuchumi pamoja na njia za kidiplomasia.

    Akizungumzia suala hilo, waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi ametoa wito kwa pande zote husika kutekeleza kikamilifu maazimio ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Na mwenzake wa Russia Bw. Sergei Lavrov amesema kutatua suala hilo kwa nguvu kutasababisha janga kwenye kanda ya kaskazini mashariki mwa Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako