• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inafanya juhudi kuhamasisha uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2017-04-27 15:33:10

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Liu Jieyi amesema China inatoa kipaumbele kwenye uvumbuzi katika mkakati wake wa maendeleo ya taifa.

    Balozi Liu ameyasema hayo jana kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Hakimilliki Duniani mjini Geneva. Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana nchini China katika shughuli za uvumbuzi, balozi Liu amesema China inatekeleza kwa pande zote mkakati wa maendeleo yanayopatikana kwa kuhimizwa na uvumbuzi, kusukuma mbele ujasiriamali na uvumbuzi wa umma, na kujumuisha kwa kina maendeleo ya sayansi, teknolojia, uchumi na jamii.

    Balozi Liu pia amejulisha kuwa idadi ya wavumbuzi wanawake wa China waliotoa maombi ya hataza ya kimataifa ilichukua nafasi ya kwanza duniani, na China itaendelea kuwaunga mkono wanasayansi wanawake kushiriki kwenye shughuli za uvumbuzi wa sayansi na teknolojia katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako