• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China atoa wito kwa vijana wa China na Afrika kuendeleza urafiki kati ya pande hizo

    (GMT+08:00) 2017-04-27 16:25:33

    Naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amehudhuria na kutoa hotuba kwenye ufungaji wa tamasha la pili la vijana wa China na Afrika lililofanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.

    Bibi Liu amesema vijana wametoa mchango muhimu kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na kwamba vijana wengi wa China wameshiriki na kuunga mkono shughuli za ukombozi na ujenzi wa nchi za Afrika.

    Bibi Liu pia amewataka vijana wa China na Afrika waeneze urafiki kati ya pande hizo nchini mwao na kuufanya urafiki huo uendelezwe katika kizazi kijacho.

    Bibi Liu pia alitembelea shule ya Confucius kwenye Chuo Kikuu cha Sayansi na Uhandisi cha Durban cha Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako