• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushirikiana na nchi nyingine kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 kupitia uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2017-04-27 16:28:28

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Liu Jieyi amesema, China iko tayari kufanya kazi na nchi nyingine ili kutekeleza Ajenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu kupitia uvumbuzi.

    Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hakimiliki, balozi Liu amesema dunia ya sasa ni kama jamii moja, na hatma ya baadaye ya dunia inategemea uvumbuzi. Ameongeza kuwa China inaendelea kusimamia ukuaji endelevu unaochochewa na uvumbuzi.

    Balozi Liu amekumbusha kuwa, China imejumuisha Ajenda ya mwaka 2030 katika Mpango wa 13 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Jamii na Uchumi, na kwamba China pia imezindua kampeni ya Uvumbuzi wa Umma na Ujasiriamali wa Umma, ambao unajumuisha hatua na sera za kuchochea ubunifu na ujasiriamali katika ngazi isiyotarajiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako