• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasikitishwa na mashambulizi ya anga ya Uturuki nchini Syria na Iraq

    (GMT+08:00) 2017-04-27 17:52:17

    Marekani imeeleza kusikitishwa na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Uturuki nchini Syria na Iraq bila ya uratibu wowote na Marekani au vikosi vya mseto.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Mark Toner amesema mashambulizi hayo hayakuidhinishwa na muungano huo wa kijeshi na kusababisha hasara kubwa kwa maisha ya askari wanaoshiriki kwenye mapambano dhidi ya IS wakiwemo wapiganaji wa kikurdi wa Pershmerga.

    Ndege za kivita za Uturuki zilifanya mashambulizi yaliyolenga maeneo ya Chama cha PKK cha Kikurdi kaskazini mwa Iraq na kusababisha vifo vya wapiganaji wasiopungua watano wa Kikurdi na kuwajeruhi wengine kumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako