• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Marekani yatangaza kanuni za kupunguza kodi

    (GMT+08:00) 2017-04-27 17:52:52

    Serikali ya Marekani imetangaza kanuni za mpango wa mageuzi ya kodi uliosubiriwa kwa muda mrefu, ambao utapunguza kwa kiwango kikubwa kodi ya mapato kwa wamarekani na makampuni.

    Mkurugenzi wa Baraza la Uchumi la Taifa la Ikulu ya Marekani Gary Cohn amesema mpango huo utapunguza idadi ya ngazi za kodi ya mapato ya mtu binafsi kutoka saba hadi tatu, na unaweza kupunguza kiwango cha juu cha kodi ya mapato ya mtu binafsi kutoka asilimia 39.6 hadi asilimia 35. Wakati huohuo, mpango huo utapunguza kiwango cha kodi ya mapato ya kampuni kutoka asilimia 35 hadi 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako