• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa mafunzo kwa watumishi wa serikali ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-04-27 18:10:43

    Watumishi 23 kutoka idara mbalimbali za serikali ya Kenya watapata mafunzo ya wiki tatu ya ujenzi wa uwezo wa watumishi nchini China.

    Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya wizara ya huduma za umma, mambo ya vijana na jinsia Simon Angote amesema kwenye hafla ya kuwaaga iliyofanyika jana mjini Nairobi, Kenya kwamba ameishukuru serikali ya China kwa kutoa nafasi hiyo ya mafunzo na anatarajia watushimi hao watakuwa na mawazo mapya baada ya kupata mafunzo nchini China, na kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini Kenya.

    Kansela wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema mwaka jana China ilitoa mafunzo kwa maofisa na mafundi 540 wa Kenya. Anatarajia kuwa watumishi hao watakaokwenda China wataongeza maelewano kuhusu China, kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika miundombinu, maendeleo ya viwanda, uwekezaji na uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako