• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanikiwa kufanya majaribio ya kuongeza msukumo katika maabara ya anga ya juu kwenye mzingo

    (GMT+08:00) 2017-04-27 19:52:02

    Chombo cha kupeleka mizigo angani cha Tianzhou-1 cha China jioni hii kimefanikiwa kufanya majaribio ya kuongeza msukumo katika maabara ya anga ya juu ya Tiangong-2 kwenye mzingo.

    Hii inamaanisha kuwa jukumu la chombo cha Tianzhou-1 limemalizika kwa mafanikio, na kwamba China imepiga hatua kubwa katika teknolojia ya kusukuma vyombo vya safari ya anga ya juu, pia kuondoa vikwazo vya kutoa nishati kwa ujenzi na uendeshaji wa muda mrefu wa kituo cha anga ya juu cha China. China imekuwa nchi ya tatu duniani inayomiliki teknolojia hii muhimu kwa kujitegemea.

    Kwa mujibu wa mpango, chombo cha Tianzhou-1 kitafanya majaribio ya pili ya kuongeza msukumo kwenye mzingo mwishoni mwa mwezi Juni, ili kuimarisha mafanikio yaliyopatikana sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako