• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuharakaisha kuboresha maeneo ya makazi ya mabanda

    (GMT+08:00) 2017-04-28 09:29:53

    Kenya inapanga kuharakisha kazi ya kuboresha maeneo ya makazi ya mabanda ili kufanya mazingira ya maisha na kazi kwenye maeneo hayo yawe mazuri zaidi.

    Akiongea kwenye maonyesho ya 25 kuhusu nyumba, katibu Mkuu wa wizara ya usafirishaji, miundo mbinu, nyumba na maendeleo ya miji Bw James Macharia amesema serikali inaandaa ramani ya kuboresha maeneo 498, na kuweka miundo mbinu muhimu. Kwenye mipango yake serikali pia inapanga kupunguza kasi ya ukuaji wa makazi ya mabanda.

    Bw Macharia amesema miji ya Kenya inakua kwa kasi, na kufanya kuwe na upungufu mkubwa wa nyumba, hali inayosababisha ongezeko la makazi ya mabanda.

    Amesema licha ya kupanuka kwa sekta ya nyumba na soko la nyumba kuchangia asilimia 11 ya pato la taifa, zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa mijini wanaishi kwenye makazi ya mabanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako