• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guterres amteua kiongozi wa timu ya uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali Syria

    (GMT+08:00) 2017-04-28 09:51:42

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amemteua Bw Edmond Mulet kutoka Guatemala kuwa kiongozi wa timu ya uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

    Habari zimesema Bw Mulet atakuwa kiongozi wa timu ya wachunguzi watatu, itakayoongoza Utaratibu wa uchunguzi wa pamoja wa Shirika linalopiga marufuku silaha za kemikali OPCW na Umoja wa Mataifa, uliozinduliwa mwaka 2015 kwa mujibu wa azimio nambari 2235 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Bw Mulet alikuwa msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani, mjumbe maalumu wa katibu mkuu na kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako