• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yaunga mkono juhudi za Tanzania kutathmini upungufu wa chakula

    (GMT+08:00) 2017-04-28 09:59:44

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetoa mfuko kuunga mkono juhudi za Tanzania kufanya tathmini ya upungufu wa chakula kote nchini.

    Tathmini hiyo ni pamoja na ukusanyaji wa data kutoka kwa wakulima ili kuhakikisha kiasi cha upungufu wa chakula nchini humo.

    Ofisa wa mpango wa FAO Bi Silvia Tirweshobwa amesema, mpango huo utatoa takwimu halisi kuhusu upungufu wa chakula, ili kuandaa mpango endelevu. Chini ya mpango huo, dola laki 3.36 za kimarekani zitatolewa kwa mradi maalumu wa majaribio, ambao maofisa kadhaa wa kilimo kutoka eneo la Morogoro watapewa mafunzo.

    Habari nyingine zinasema, mifugo elfu 6 hivi wamekufa kutokana na ukame katika mkoa wa Shinyanga, kuanzia mwezi Septemba mwaka jana hadi Februari ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako