• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza "ujasiriamali na uvumbuzi wa umma"

    (GMT+08:00) 2017-04-28 17:14:32

    Kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimepitisha azimio la kuadhimisha "Siku ya Uvumbuzi Duniani" na kuzitolea mwito nchi mbalimbali kuunga mkono ujasiriamli na uvumbuzi wa umma.

    Akizungumza baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Liu Jieyi amesema, serikali ya China inafuata kwa kina mawazo ya maendeleo ya "uvumbuzi, uratibu, kijani, uwazi na kunufaika kwa pamoja", kuufanya uvumbuzi uwe sehemu muhimu ya mikakati ya maendeleo ya taifa, na kuhimiza "ujasiriamali na uvumbuzi wa umma". Ameongeza kuwa kupitishwa kwa azimio hilo kumeonesha kuwa China imechangia mpango wake kwa jumuiya ya kimataifa katika ukuaji wa uchumi na kutengeneza nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako