• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNIDO yasema pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litasaidia utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka wa 2030

    (GMT+08:00) 2017-04-28 17:15:19

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO Li Yong amesema pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lina maana kubwa kwa utekeleza wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka wa 2030 ya Umoja wa Mataifa.

    Akihojiwa na waandishi wa habari aliposhiriki Maonyesho ya Viwanda mjini Hannover, Ujerumani, Bw. Li amesema pendekezo hilo lililotolewa na serikali ya China sio tu linaziunganisha nchi zinazohusika katika sekta za uchumi, biashara na uwekezaji, pia linahimiza maendeleo ya biashara duniani na kuondoa athari mbaya zinazotokana na msukosuko wa kifedha wa mwaka 2008. Ameongeza kuwa lengo la kimsingi la Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka wa 2030 ya Umoja wa Mataifa ni kuondoa umaskini, na njia bora ya kuondoa umaskini ndio maendeleo ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako