• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Usalama leo kujadili suala la nyuklia la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-04-28 17:50:16

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi atahudhuria mkutano wa wazi wa ngazi ya mawaziri kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea utakaofanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo huko New York.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema mkutano huo unatakiwa kutoa kipaumbele katika kujadili jinsi ya kutuliza hali ya wasiwasi ya hivi sasa katika Peninsula ya Korea, na kulinda amani na utulivu wa Peninsula hiyo.

    Kabla ya mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alikutana na naibu waziri wa mambo ya nje ya Russia Bw. Gennadiy Gatilov. Bw. Wang Yi alisema hivi sasa mvutano katika Peninsula ya Korea umeongezeka na kuna hatari ya kutodhitibiwa. China inapendekeza pande husika kushikilia kanuni ya kuifanya Peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia na kubadilisha mfumo wa kusimamisha vita kuwa mfumo wa kutimiza amani. Pande mbili zinaona kuwa pande husika zinatakiwa kutekeleza kikamilifu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo, na kuchukua hatua kuzuia mchakato wa makombora ya nyuklia nchini Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako