• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kenyatta aipongeza serikali ya China kwa msaada wake kukuza nishati ya mvuke

    (GMT+08:00) 2017-04-29 17:24:10

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana aliipongeza serikali ya China kwa msaada wake wa kuongeza nguvu ya uzalishaji wa nishati ya mvuke nchini humo.

    Akiongea huko Naivasha wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa nishati wa Olkaria V ambao utazalisha umeme megawati 158, Kenyatta aliishukuru serikali ya China kwa kuongeza fedha na wataalamu ambao wameifanya Kenya kuwa wazalishaji wanaoongoza wa umeme wa mvuke. Kenyatta pia ameidhinisha vitengo 14 vya visima vitakavyozalisha umeme jumla ya megawati 75.

    Benki ya Uzaji na uagizaji nje ya China imetoa mkopo wa dola milioni 400 za Kimarekani kuifanya Kenya iweze kuchimba visima 80 vya nishati hiyo ya mvuke lakini kutokana na utaalamu wa kampuni ya China hadi sasa vimechimbwa visima 89.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako