• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la kupiga marufuku silaha za kemikali lasisitiza kufanya juhudi ya kuondoa tishio la silaha hizo

    (GMT+08:00) 2017-04-29 18:16:39

    Mkurugenzi mkuu wa shirika la kupiga marufuku silaha za kemikali Bw. Ahemt Umzucu jana alisema, tangu kusainiwa kwa kanuni ya kupiga marufuku silaha za kemikali na kuundwa kwa shirika hilo miaka 20 iliyopita, jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa katika kuondoa tishio la silaha hizo, lakini katika miaka ya hivi karibuni matukio ya kutumia silaha za kemikali yametokea tena, na kwamba watu wenye msimamo mkali huenda wakafanya mashambulizi ya kigaidi kwa kutumia silaha za kemikali. Amezitaka pande husika kuendelea kuimarisha ushirikiano ili kuzuia na kukabiliana na tishio la silaha za kemikali na kuondoa tishio hilo kabisa.

    Bw. Umzucu alisema, nchi 192 zimesaini kujiunga na kanuni ya kupiga marufuku silaha za kemikali. Miongoni mwa shehena ya silaha za nyuklia zilizoripotiwa, asilimia 95 zimeangamizwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako