• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ICRC yasaidia familia 55,000 za Somalia kukabiliana na ukame

    (GMT+08:00) 2017-04-29 18:16:55

    Taarifa iliyotolewa jana na Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC inasema, familia zinazokabiliwa na ukame zimepata msaada wa dola za kimarekani 100 kila moja ili kukabiliana na changamoto hiyo.

    Kamati hiyo imetoa fedha hizo kwa familia zaidi elfu 55 karibu na Baidoa ili kuzisaidia kukabiliana na ukame katika kipindi cha dharura. Na familia zenye hali ngumu zaidi zitapata duru tatu ya misaada ya kifedha kupitia simu za mkononi.

    Hali ya ukame nchini Somalia imewafanya watu zaidi milioni 6 wawe na hatari ya utapiamlo na kusababisha watu wengi kupoteza makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako