• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Kenya yasema watu wawili wameuawa, 63 wamekamatwa katika mchujo wa chama

    (GMT+08:00) 2017-04-30 19:08:47

    Polisi nchini Kenya ilisema watu wawili tu wameuawa na wengine 63 walikamatwa kwa makosa mbalimbali ya uchaguzi wa awali nchini humo.

    Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett amesema kati ya Aprili 23 na 24, kesi ishirini na nne ziliripotiwa kwenye kaunti tofauti wakati uchaguzi huo wa awali ulikuwa ukifanyika.

    Mkuu huyo wa polisi amewataka wakenya kuendelea kuimarisha amani katika kipindi kinachofuata cha uchaguzi kulingana na kalenda ya uchaguzi.

    Katika mchujo wa awali ndani ya vyama vya upinzani na chama tawala ulioanza wiki iliyopita, kumekuwa na matukio ya machafuko na shutuma za wizi wa kura. Chama tawala cha Jubilii kimeahirisha kuanza mchujo kutokana na uhaba wa vifaa vya kupigia kura.

    Wanamgambo wa kikundi cha Al-Qaeda, Al-Shabaab, wametishia kulipiza kisasi kwa kushambulia Kenya, wakishutumu vikosi vya Kenya kuvuka mipaka na kupunguza harakati zao na kusaidia Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako