• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa umesema mkutano wa London ni muhimu kwa mageuzi ya Somalia

    (GMT+08:00) 2017-04-30 19:09:59

    Muwakilishi maalimu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amesema mkutano wa kimataifa utakaofanyika Mei 11 nchini Uingereza unatarajiwa kuwa ni muhimu kwa kasi ya mageuzi ya somalia ya hali ya usalama inayoendelea, mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.

    Kwa mujibu wa Keating, mkataba wa maafikiano ya mkutano huo katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na usalama wa mkataba, msaada kwa ajili ya ukame, ahueni ya kiuchumi na vipaumbele vya siasa ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba na mchakato wa demokrasia utakaowezesha mtu mmoja na kura moja katika uchaguzi mwaka 2020.

    Mkutano utashirikisha viongozi waandamizi kujadili kiwango cha juu cha msingi na kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Somalia na washirika wake wa kimataifa.

    Hivi karibuni washiriki walisifu makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa na serikali na viongozi wa juu wa jimbo wa nchi kwa usanifu mpya wa majeshi ya Somalia kwa ajili ya usalama wa taifa hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako