Korea kaskazini imesema luteka ya pamoja ya Marekani na Korea kusini, na Marekani kuweka zana za kinyuklia kwenye peninsula ya Korea ni chanzo cha kuongezeka kwa mvutano kwenye kanda hiyo. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. Han Song Ryol amesema nchi yake itachukua hatua imara kuendeleza uwezo wake wa kinyuklia ili kulinda mamlaka, haki zake, na amani ya peninsula hiyo, kutokana na tishio la Marekani kuanzisha vita vya kinyuklia dhidi ya Korea Kaskazini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |