• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutumia mashindano ya Kriketi ya India kutangaza utalii

    (GMT+08:00) 2017-05-01 09:20:18

    Bodi ya Utalii ya Kenya KTB imesema itatumia msimu wa kriketi unaoendelea nchini India kutangaza bidhaa zake za utalii na kuongeza hamasa ya watu kutaka kutembelea Kenya.

    Bodi hiyo imetenga takriban dola za kimarekani laki mbili na nusu kwa ajili ya kutafuta soko na kufanya kampeni za kuitangaza nchi hiyo, ikisihirikiana na timu moja ya ligi ya kriketi ya India (The Rising Pune Super Giants RPS).

    Kwenye taarifa yake Mkurugenzi mkuu wa KTB Betty Rader amesema wanatarajia ushirikiano huo na timu inayoongoza kwenye ligi kuu ya Kriketi ya India utaipa nafasi Kenya kuwa sehemu itakayotembelewa na mashabiki wa kriketi wa India. Kupitia ligi hiyo iliyoanza mwezi Aprili na kumalizika mwishoni mwa Mei, Kenya inatarajia kunufaika kwa kutangazwa katika zaidi ya nchi 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako