• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 352 wauawa katika mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani dhidi ya IS

    (GMT+08:00) 2017-05-01 09:54:17

    Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema raia wasiopungua 352 wameuawa katika mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani dhidi ya Kundi la IS nchini Iraq na Syria kuanzia mwezi Agosti mwaka 2014 hadi mwezi Machi mwaka huu.

    Wizara hiyo imesema bado inaendelea kupitia ripoti 42 za vifo vya raia. Kwa mujibu wa wizara hiyo raia 45 wameuawa tangu mwezi Novemba mwaka jana hadi mwezi Machi mwaka huu.

    Aidha, jeshi la Marekani limeripoti vifo vya raia 80 tangu mwezi Agosti mwaka 2014 hadi sasa, ambavyo havikutangazwa awali.

    Wizara hiyo pia imesema jeshi la muungano linafanya juhudi kupunguza hatari kwa raia, lakini haliwezi kuepusha kabisa vifo au majeruhi ya raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako