• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi zaidi ya 200 wauawa katika mapambano ya ndani mashariki mwa Damascus, Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-01 10:31:01
    Waasi zaidi ya 200 wameuawa katika mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa siku tatu kati ya makundi ya Jaish al-Islam na Nusra Front, yakigombea udhibiti wa eneo la Ghouta Mashariki, pembezoni mwa Damascus.

    Habari zinasema kundi la Jaish al-Islam linaloungwa mkono na Saudi Arabia lilianza mashambulizi dhidi ya kundi la Nusra Front linaloungwa mkono na Qatar na kusababisha vifo vya raia wasiopungua watano.

    Huku, watu takriban 3,000 waliandamana huko Ghouta Mashariki wakizitaka pande hizo mbili zisitishe mapambano, ambapo kundi la Jaish al-Islam liliwafyatulia risasi na kuwatimua.

    Wachambuzi wanaona kuwa mapigano hayo yameakisi mgongano wa maslahi ya pande zinazoyaunga mkono makundi hayo, ambapo yote yanagombea udhibiti imara wa maeneo ya mashariki wa Damascus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako