• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Ulaya wafikia mwongozo wa kuzungumza na Uingereza kuhusu BREXIT

  (GMT+08:00) 2017-05-01 15:26:05

  Umoja wa Ulaya jana umefanya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama 27 isipokuwa Uingereza, na kujadili mazungumzo na Uingereza kuhusu Brexit. Mwenyekiti wa baraza la Ulaya Donald Tusk amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, nchi hizo 27 zimeafikiana kuhusu mwongozo wa kuzungumza na Uingereza.

  Bw. Tusk amesema viongozi wa nchi hizo 27 wameonyesha mshikamano mkubwa, na kupitisha waraka wa mwongozo kwa haraka. Pia amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya utafanya mazungumzo na Uingereza kwa vipindi mbalimbali, hii ina maana kuwa kabla ya kuzungumzia uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza, pande hizo mbili zitapata maendeleo kwanza katika masuala ya haki na maslahi ya wananchi, mambo ya fedha na mipaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako