• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vitabu vinne vya China vyachapishwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-01 16:27:59

    Serikali ya Kenya imeruhusu kuchapishwa kwa vitabu vinne vilivyotolewa na kundi la uchapishaji la Changjiang la China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa vitabu vya China kuchapishwa kwa namba vipimo viwili vya kimataifa vya China na Kenya.

    Kitabu cha "Hadithi za watu 60 kutoka China na Afrika " kinaonesha maendeleo ya China na Afrika kwenye siasa, uchumi, diplomasia, utamaduni, teknolojia, elimu na uhifadhi wa mazingira katika miaka 60 iliyopita kupitia simulizi za watu 60 kutoka China na Afrika.

    Vitabu vya "Atlasi ya Jiografia ya Kenya" na "Mimea ya kawaida nchini Kenya" ni mafanikio ya ushirikiano kati ya taasisi ya sayansi na teknolojia ya China na wataalamu wa Kenya kwenye mazingira ya maliasili na uhifadhi wa aina nyingi za Baiolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako