• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watano wauawa katika mapigano kati ya jamii za Pokot na Turkana, kusini magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-01 19:08:16

    Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa watu watano wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya jamii zaPokot na Turkana, kusini magharibi mwa Kenya.

    Kamishna wa kaunti ya Baringo Peter Okwanyo amesema usalama umeimarika katika jimbo la Turkana na Baringo baada ya watuhumiwa waliokuwa na silaha kutoka kabila la Pokot kuua mtu mmoja Ijumaa iliyopita katika Lokori, Turkana na kuiba wanyama kadhaa.

    Amesema kikosi cha usalama kimetumwa kwenye sehemu hiyo kukamata watuhumiwa wa shambulizi hilo na kurejesha hali ya utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako