• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Muntari abaguliwa Italia, mwamuzi amtwanga kadi ya njano, yeye aamua kutoka nje wakati mechi ikiendelea

  (GMT+08:00) 2017-05-02 09:00:44

  Kiungo Mghana Sulley Muntari amekutana na tabia zisizofaa katika michezo zinazopaswa kulaaniwa za ubaguzi akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu maarufu Serie A jana wakati akiichezea Pescara dhidi ya Cagliari ambayo mashabiki wa timu hiyo walimbagua Muntari ambaye alilazimika kutoka nje ya uwanja.

  Muntari alilazimika kumfuata mwamuzi na kumueleza kilichokuwa kinatokea ili asimamishe mchezo kama sheria zinavyoeleza, lakini mwamuzi aligoma na kumpa kadi ya njano.

  Kitendo hicho kilimuudhi zaidi na Muntari aliyewahi kung'ara na AC Milan, akaamua kutoka nje na kuiacha timu yake ikiwa na wachezaji pungufu uwanjani.

  Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa Cagliari kuonyesha ubaguzi wa wazi, waliwahi kufanya hivyo kwa Samuel Et'oo mwaka 2010 wakati akiichezea Inter Milan, mwamuzi alisimamisha mchezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako