• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Belarus zasaini makubaliano ya uchimbaji na utafutaji wa madini

    (GMT+08:00) 2017-05-02 09:10:35

    Sudan na Belarus zimesaini makubaliano ya ushirikiano yanayohusu uwekezaji kwenye sekta ya madini, viwanda na kilimo.

    Makubaliano hayo yamesainiwa na waziri wa madini wa Sudan Bw Ahmed Al Karouri, na waziri wa maliasili na ulinzi wa mazingira wa Belarus.

    Mkurugenzi wa mamlaka ya Jiolojia ya Sudan Bw Mohamed Fatma Abdallah amesema makubaliano yaliyosainiwa pia yanahusu uwekezaji, mafunzo kuhusu mazingira, uendelezaji wa maabara, ushirikiano kwenye mambo ya sheria na uingizaji wa teknolojia mpya.

    Makampuni 461 yanafanya kazi kwenye sekta ya madini nchini Sudan, ambayo inachangia asilimia 40 ya bidhaa za Sudan zinazouzwa nje. Mwaka jana uzalishaji wa dhahabu wa Sudan ulipanda na kufikia tani 93.4 na kuwa ya pili kwa uzalishaji wa dhahabu barani Afrika baada ya Afrika kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako