• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi ya Ghana yaitaka serikali kupitisha mikataba kuhusu afya na usalama kazini

    (GMT+08:00) 2017-05-02 09:10:52

    Taasisi ya kusimamia hali ya afya na usalama kazini nchini Ghana, imeitaka serikali ya nchi hiyo kupitisha makubaliano ya shirika la kazi duniani ILO ili kulinda afya na usalama wa wafanyakazi nchini Ghana.

    Taarifa iliyotolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi, mkuu wa ILO Bw. Francis Ahadzi amesema ana wasiwasi kuhusu Ghana kushindwa kupitisha mikataba ya ILO kuhusu afya na usalama wa wafanyakazi kazini.

    ILO imekadiria kuwa watu milioni 2.3 hufa kila mwaka kutokana ajali na magonjwa yanayohusiana na kazi.

    Taasisi ya kusimamia hali ya afya na usalama kazini nchini Ghana imewakumbusha waghana kuwa hali ya afya na usalama kazini ni jukumu la pamoja na ni haki ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako