• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yaitaka jumuiya ya kimataifa ihimize mchakato wa amani kati yake na Israel

    (GMT+08:00) 2017-05-02 09:50:47
    Msemaji wa Ikulu ya Palestina ametoa taarifa akiitaka jumuiya ya kimataifa itumie fursa kuhimiza mchakato wa amani kati yake na Israel.

    Taarifa inasema rais Mahmoud Abbas wa Palestina kesho atakutana na mwenzake wa Marekani Donald Trump, ambapo atasisitiza umuhimu wa haki na amani kwenye kushughulikia suala hilo katika msingi wa "ufumbuzi wa kuwepo kwa nchi mbili" na pendekezo la amani la nchi za kiarabu.

    Habari nyingine zinasema, Kundi la Hamas limetoa waraka mpya wa kisiasa, likieleza kuwa linakubali kuanzishwa kwa nchi ya Palestina kutokana na mipaka iliyokubaliwa mwaka 1967 kwenye ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza, lakini bado inashikilia msimamo wake wa kutoitambua Israel na itaendelea kupambana na uvamizi wa ardhi ya Palestina, licha ya kuwa inawaheshimu wayahudi na makabila mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako