• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wazialika Sudan na Sudan Kusini kujadili masuala ya usalama

    (GMT+08:00) 2017-05-02 10:00:25

    Umoja wa Afrika umezialika Sudan na Sudan Kusini kuhudhuria mkutano wa Addis Ababa kujadili masuala ya usalama kati ya nchi hizo mbili.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amesema, kamati ya pamoja kuhusu siasa na usalama kati ya Sudan na Sudan Kusini imepokea mwaliko kutoka kwa mkuu wa jopo la watalaamu wa ngazi ya juu la Umoja wa Afrika AUHIP Bw. Thabo Mbeki.

    Amesema, jopo la wataalamu litaitisha mkutano Mei 8 na 9 huko Addis Ababa kujadili nyaraka kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya usalama, ikiwemo uwekaji mipaka, eneo lisilo na shughuli za kijeshi, na nyaraka kuhusu kuyahifadhi na kuyaunga mkono makundi yenye silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako