• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la China la "Ukanda mmoja, Njia moja" lahimiza kuanzishwa kwa mustakabali wa pamoja wa binadamu

    (GMT+08:00) 2017-05-02 18:49:34

    Pendekezo la China la "Ukanda mmoja, Njia moja" limekuwa msukumo muhimu wa kuhimiza maendeleo ya jumuiya ya kimataifa. Mkurugenzi wa Taasisi ya uchunguzi wa mambo ya Asia na utandawazi katika taasisi ya sera za umma ya Lee Kuan Yew katika Chuo Kikuu cha Taifa la Singapore Bw. Huang Jing, ameeleza kuwa pendekezo hilo litatoa fursa ya maendeleo kwa pande zote zinazojiunga na pendekezo hilo, na kutoa mazingira salama na yenye utulivu kwa China.

    Mkutano wa kilele wa baraza la kimataifa la "Ukanda mmoja, Njia moja" utafanyika kati ya tarehe 14 hadi 15 Mei mjini Beijing, Profesa Huang Jing amealikwa kuhudhuria baraza la wataalamu mashuhuri. Alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Radio China Kimataifa alisema, pendekezo hilo ni mkakati mkubwa, ambao utakuwa na manufaa kwa China katika maendeleo ya uchumi na usalama wa kimkakati.

    Profesa Huang anaona kuwa, hivi sasa China inakabiliana na changamoto kubwa mbili, kwanza ni namna ya kutimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa, nyingine ni athari mbaya zinazoletwa na mkakati uliotolewa na serikali ya Obama kuhusu kutimiza tena uwiano katika eneo la Asia na Pasifiki. Profesa Huang anaona pendekezo hilo la "Ukanda Mmoja, Njia moja" la China litatoa majibu kwa changamoto hizo. Anasema:

    "Lengo la utoaji wa pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' ni kukabiliana na changamoto hizo mbili. Hivi sasa China ni nchi kubwa ya kwanza ya biashara duniani ambayo ina ushawishi mkubwa duniani, rais Xi amegundua kuwa maendeleo ya nchi jirani yanaweza kuhimiza kwa hatua halisi maendeleo ya China, na tatizo kubwa linalokwamisha maendeleo ya nchi jirani ni kuwa nyuma kwa ujenzi wa miundo mbinu."

    Profesa Huang anaona kuwa, nchi zilizoendelea duniani zilijiendeleza kiuchumi kwa kufuata kanuni moja ya kuendeleza ujenzi wa miundo mbinu. Kwa mujibu wa utafiti wake, ujenzi wa miundo mbinu vilevile umetoa mchango muhimu kwa maendeleo ya China. Anaona kuwa miradi ya pendekezo hilo la China si kama tu inasaidia nchi nyingine, bali pia itahimiza maendeleo ya uchumi wa China yenyewe.

    Profesa Huang pia anaona kuwa maendeleo ya "Ukanda mmoja, Njia moja" yataisaidia China kupata msukumo mpya kwa uchumi wa China, na kuhimiza kukua kwa viwanda mbalimbali nchini China, pia litasaidia China kukabiliana na changamoto za usalama. Anasema:

    "Pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' ni mpango wa maendeleo unaonufaisha pande zote zinazohusika, na kuziwezesha nchi mbalimbali na China ziwe na umoja thabiti wa uchumi wenye maslahi ya pamoja, na kuendeleza usalama wa ushirikiano na usalama wa pamoja. Kutokana na umoja huo, maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali yana uhusiano. Na utulivu ni sharti la lazima kwa maendeleo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako