• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Sekta ya utalii yakuwa

    (GMT+08:00) 2017-05-02 19:22:41

    Soko la utalii nchini Tanzania linakua kwa kasi sana , ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kutokana na vivutio na huduma.

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania imekuwa na soko kubwa la utalii katika jumuiya ya Afrika Mashariki

    Mwaka jana Tanzania ilipata watalii milioni 1,218,000 na Wakenya walipata 1.3 na nchi zingine zilipata wachache.

    Akizungumzia kuhusu tuzo hizo, alisema zimetolewa kwa hoteli zenye ubora wa huduma na zimepewa nyota kulingana na madaraja yao kuanzia nyota moja hadi tano.

    Waziri amesisitiza wafanyikazi na wamiliki wa mahoteli kuboresha wa huduma zao.

    Amesema huduma bora ndizo zinawafanya wataalii kuwa mabalozi wazuri, wanaporudi kwao na kueleza wamekutana na huduma nzuri na malazi mazuri hivyo kuwavutia wenzao.

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii (TCT), Abdulkadir Mohamed alisema wamefanya tathmini hiyo ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma kulingana na uwezo wake sambamba na kuwapatia watalii huduma bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako