• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuwa mwenyeji wa baraza Afrika na Asia la sheria za kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-05-03 09:08:06

    Kenya yawa mwenyeji wa baraza la Afrika na Asia linalojadili changamoto za sheria za kimataifa.

    Naibu Rais wa Kenya Bw William Ruto ameliambia baraza hilo kuwa pande mbili zimekubaliana kuhimiza ushirikiano kati yao ili kulinda maslahi yao.

    Amesema pande hizo zitashirikiana kukabiliana na matishio yaliyopo na matishio mapya kwa kuimarisha ushirikiano kwenye sheria za kimataifa. Pia ametoa mwito kwa serikali za nchi za Asia na Afrika kushirikiana kwenye masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja, kwani historia imeonyesha kuwa, pande hizo mbili zinaposhirikiana zinaweza kuwa na nguvu ya ushawishi kwa dunia.

    Hii ni mara ya tatu tangu mwaka 1970 kwa Kenya kuwa mwenyeji wa baraza hilo linalofanyika kwa muda wa siku tano, likiwakutanisha pamoja maofisa waandamizi wa serikali na watunga sera kutoka nchi 47.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako