• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaanza kuboresha barabara mjini Kigali

    (GMT+08:00) 2017-05-03 09:08:25

    Kampuni ya China imeanza kazi ya kuboresha barabara za mji wa Kigali, inayotarajiwa kufanya hali ya jumla ya usafiri mjini humo kuwa nzuri.

    Mradi huo utakaohusisha barabara za kilomita 54 unagharamiwa na Benki ya Exim ya China kwa mkopo wenye upendeleo maalum, ambao licha ya kuboresha huduma za usafiri pia unatarajiwa kuhimiza sekta ya utalii na kuendeleza uchumi.

    Mji wa Kigali unaendelea kukua kwa kasi na wakazi wengi wanahamia kwenye mji huo, mradi huo utasaidia kupanua barabara za mji ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu.

    Mhandisi wa mji wa Kigali Bw Nkurunziza Alphonse amesema kazi kwa sasa inaendelea vizuri, na mradi huo unatarajiwa kuboresha eneo la kati la mji, na kuongeza nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako