• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaandaa mazungumzo ya Kusini na Kusini kuharakisha mapambano dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2017-05-03 09:10:36

    Maofisa wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi tajiri na maskini.

    Wito huo umetolewa kufuatia mkutano wa Kusini na Kusini na Ushirikiano wa Pande tatu wa Maendeleo Endelevu, unaowashirikisha wajumbe kutoka Asia, Amerika Kusini, Amerika Kaskazini, Japan, Korea Kusini na Afrika Magharibi, wanaojadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa. Waziri wa Mipango wa Kenya Bw Mwangi Kiunjuri amesema ushirikiano wa kusini na kusini, ulioanza baada ya mkutano wa Bandung ambao ni jukwaa kubwa la ushirikiano wa Asia na Afrika, unapaswa kuendeleza mafanikio ya malengo ya kutokomeza umaskini ya Umoja wa Mataifa. Waziri Kiunjuri amesema Malengo ya 2030 ni ajenda ya mageuzi ya nchi kuelekea kuboresha maisha ya watu, kuzalisha mali na kuwa nchi yenye nguvu ya ushindani duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako