• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na Ujerumani zajadili ushirikiano na masuala ya Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-03 09:30:43

    Naibu chansela wa Ujerumani na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw Sigmar Gabriel amekutana na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahmat mjini Addis Ababa, Ethiopia na kuzungumzia ushirikiano kati ya nchi zao na masuala ya bara la Afrika.

    Pande hizo mbili zimeshauriana kuhusu masuala ya amani, usalama, na mengineyo yanayofuatiliwa zaidi barani Afrika. Pia zimejadili mapendekezo kuhusu Afrika chini ya uenyekiti wa Ujerumani wa kundi la G20 mwaka huu.

    Habari zinasema pande hizo mbili pia zimejadiliana kuhusu hali ya Somalia na mkutano kuhusu suala la Somalia utakaofanyika mwezi huu mjini London, Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako