• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Russia wajadili mgogoro wa Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-03 09:44:47

    Ikulu ya Marekani imesema Rais Donald Trump wa Marekani amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kuhusu mgogoro wa Syria, mapambano dhidi ya ugaidi kwenye Mashariki ya Kati pamoja na hali ya Peninsula ya Korea.

    Taarifa ya Ikulu ya Marekani imesema kwenye mazungumzo marais hao wamejadili ushirikiano zaidi kwenye mapambano dhidi ya ugaidi kanda ya Mashariki ya Kati. Taarifa pia imesema Serikali ya Marekani itatuma mjumbe katika mazungumzo ya kusimamisha vita yatakayofanyika leo na kesho mjini Kazakhstan.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Trump na Putin kufanya mazungumzo kwa njia ya simu, baada ya nchi hizo kuzozana kutokana na Marekani kuishambulia Syria mwezi uliopita kwa tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako