• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya na Somalia kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi

  (GMT+08:00) 2017-05-03 10:12:26

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema uhusiano wa karibu kati ya Kenya na Somalia utaziwezesha nchi hizo mbili kukabiliana kwa pamoja na tishio la ugaidi na changamoto nyingine.

  Rais Kenyatta amezitaka nchi hizo mbili ziimarishe uratibu katika juhudi za kuzidisha amani, pia amempongeza rais Mohamed wa Somalia kwa juhudi zake za kulinda amani. Rais Kenyatta amesema Kenya inapenda kushirikiana na Somalia katika kuhimiza biashara kati ya nchi mbili.

  Habari pia zinasema kiongozi mwandamizi wa waasi wa Kundi la Al-Shabaab Abdirim Sheikh Hassan jana alijisalimisha kwa vikosi vya jimbo la Jubaland mjini El-Wak, eneo la Gedo kusini mwa Somalia, na kuwa mfuasi wa 12 wa kundi hilo kujisalimisha kwa serikali ya Somalia katika wiki mbili zilizopita baada ya rais wa Somalia kutoa msamaha kwao endapo wataweka chini silaha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako