• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyekuwa rais wa Zambia atarajia kutoa mchango tena kwa ajili ya ukarabati wa reli ya TAZARA

    (GMT+08:00) 2017-05-03 17:22:19
    Reli ya Tazara inayounganisha Tanzania na Zambia inakumbwa na matatizo mawili ya ukosefu wa abiria na upungufu wa utaratibu wa usimamizi. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipotembelea Zambia mwanzoni mwa mwaka huu alisema, China, Tanzania na Zambia zimeafikiana kuhusu kukarabati reli hiyo. Je, sasa mpango wa ukarabati huo unaendeleaje? Reli hiyo itachangia vipi katika utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja"?

    Aliyekuwa rais wa kwanza wa Zambia Bw. Kenneth Kaunda mwenye umri wa miaka 93 anaishi umbali wa nusu saa kwa gari kutoka kusini mashariki mwa Lusaka. Akiwa mwanzilishi wa mpango wa ujenzi wa Reli ya Tazara anafuatilia sana hali ya reli hiyo baada ya kustaafu kwa karibu na miaka 20. Akizungumzia mustakabali wa reli hiyo anasema:

    "Natarajia kuziwezesha nchi nyingine kufanya biashara na China kama nchi yangu ilivyo hivi sasa kupitia reli ya Tazara. Tunaweza kupanua reli hiyo ili kuunganisha nchi nyingine katika kanda hiyo na China."

    Matarajio hayo ya Bw. Kaunda yanalingana na lengo la pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" lililotolewa na serikali ya China ambalo linatafuta mawasiliano ya sera, miundo mbinu, biashara, fedha na mioyo ya wananchi kati ya nchi mbalimbali zilizojiunga na pendekezo hilo, ili kuziwezesha zinufaike kwa pamoja na fursa za maendeleo ya China na kupata ustawi wa pamoja. Balozi wa China nchini Zambia Bw. Yang Youming anasema:

    "Katika miaka 40 iliyopita, reli ya Tazara imesafirisha abiria zaidi ya milioni 50, zaidi ya tani milioni 30 za mizigo, na kuchangia sana katika maendeleo ya Zambia na mawasiliano ya watu kati ya Zambia na nchi jirani. Vilevile imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuwaandaa wataalamu wa Zambia. Wakati reli hiyo ilipojengwa, mafundi wa China na Zambia walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja, hayo ni mawasiliano ya watu, na pia Zambia ilituma watu 100 kusoma nchini China, na baadaye iliendelea kutuma watu kadhaa nchini China kila mwaka. Watu hao walirudi Zambia na kushughulikia uendeshaji wa reli na sekta nyingine na kuwa wataalamu wanaochangia maendeleo ya Zambia."

    Ukarabati wa reli ya Tazara ukiwa sehemu ya utekelezaji wa pendekezo la China la "Ukanda mmoja, Njia moja",utahimiza mawasiliano kati ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika, na kati ya kusini na mashariki ya Afrika. Nchi tatu za China, Tanzania na Zambia zimeafikiana kukarabati reli ya Tazara. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipotembelea Zambia mwanzoni mwa mwaka huu alifafanua kihalisi mpango wa ukarabati wa reli hiyo: Kufanya mageuzi kwa pande zote katika utaratibu wa usimamizi wa reli hiyo ili kuunganisha reli na bandari, kujenga maeneo ya uchumi ya viwanda yaliyopo katika ukanda huo, ili kuhimiza Zambia na Tanzania pamoja na nchi nyingine katika kanda hiyo kuharakisha maendeleo ya viwanda, na kutimiza ushirikiano na ustawi katika mambo ya kisasa ya kilimo.

    Bw. Kaunda ameeleza kuwa anatarajia kutembelea China kwa ajili ya mambo ya reli ya Tazara.

    "Mradi kama reli ya Tazara unazinufaisha pande zote husika, na kuchangia katika mawasiliano kati ya Zambia na China. Kutia uhai mpya kwenye reli hiyo kuna umuhimu mkubwa, napenda kutembelea China tena kwa ajili ya mambo ya ukarabati wa reli hiyo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako