• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapata mafanikio katika kuinua maendeleo ya watu

    (GMT+08:00) 2017-05-03 17:28:35

    Kenya imepata mafanikio makubwa katika kuendeleza ustawi na ubora wa maisha, na kuzishinda nchi nyingine za Afrika kusini mwa Sahara.

    Matokeo ya utafiti wa alama ya Maendeleo ya Watu kwa mwaka 2016 uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) yameonyesha kuwa, Kenya imeshika nafasi ya 146 kati ya nchi 188 zilizofanyiwa utafiti huo, ikifuatiwa na Tanzania iliyochukua nafasi ya 151 na Cameroon nafasi ya 153.

    Ripoti hiyo imesema, wakati Kenya ikionyesha maendeleo katika kuboresha upatikanaji wa elimu, afya na usafi, watu wengi zaidi wanaondokana na umasikini, na watu wachache wanakabiliwa na uhaba wa chakula, bado kuna tofauti katika maeneo ya mijini na vijijini, na pia kati ya wanaume na wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako