• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Russia wazungumzia suala la Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-03 18:24:15

    Rais Donald Trump wa Marekani amewasiliana kwa simu na rais Vladimir Putin wa Russia, ambapo viongozi hao wamejadiliana kuhusu suala la Syria.

    Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imesema, marais hao wamesisitiza kwa pamoja kuwa pande mbalimbali zinatakiwa kufanya juhudi ili kukomesha matumizi ya kimabavu. Pia marais hao wamejadili suala la uanzishaji wa eneo la usalama, ili kusuluhisha mgogoro wa kibinadamu nchini Syria.

    Habari nyingine zinasema, kambi moja ya wakimbizi iliyoko kaskazini mashariki mwa Syria jana imeshambuliwa na wapiganaji wa kundi la IS, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako