• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema utatuzi wa kisiasa ni njia sahihi pekee ya kutatua mgogoro wa Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-03 19:05:42

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, njia ya kisiasa ndio njia sahihi ya kutatua mgogoro wa Syria.

    Bw. Geng Shuang amesema, China inaitaka jumuiya ya kimataifa itumie fursa ya mkutano wa Astana kuhusu Syria unaofanyika kuanzia leo kuimarisha mawasiliano, kuonesha moyo dhati, kuongeza uaminifu, na kutoa mchango kwa kuhimiza mchakato wa utatuzi wa suala la Syria kwa njia ya kisiasa.

    Pande mbalimbali za mkutano huo wa siku mbili hazijafikia maafikiano kuhusu masuala kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako