• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: kuwekeza katika viwanda kupatiwa ardhi za bure bila kuchelewa.Museveni asema

    (GMT+08:00) 2017-05-03 19:53:57

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amegiza wawekezaji wanaoangalia kuwekeza katika viwanda kupatiwa ardhi za bure bila kuchelewa.

    Museveni amesema kutoa ardhi bure kwa wakezaji itakuza sekta ya viwanda, ambayo, kwa upande mwengine, itatatua swala la ukosefu wa ajira.

    Akizungumza katika uzinduzi wa Sunbelt Textile Company katika mjini Jinja wiki hii, Rais amesema wawekezaji ambao wanataka kuanzisha biashara na makampuni wanapaswa kupatiwa ardhi ya bure bila kuchelewa, huku akisema Waganda watakuwa walengwa wakuu.

    Aidha amesema ni Uchumi wa Uganda utapoteza kama Waganda wataifanya vigumu kwa wawekezaji kufanya kazi nchini humu.

    Pia amesema wawekezaji katika sekta nne zilizopewa kipaumbele na serikali; sekta ya madini, sekta ya utalii, sekta ya kilimo na sekta ya usindikaji na sekta ya teknolojia na mawasiliano watapata ardhi za bure.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako