• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanakijiji 7,000 wafaidi mradi wa maji Sikonge

    (GMT+08:00) 2017-05-03 19:54:15

    Wakazi zaidi ya 7,000 katika kijiji cha Kiyombo wilayani Sikonge, mkoani Tabora wameanza kunufaika na mradi wa maji ya kisima kirefu baada ya halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha ujenzi wake.

    Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo, Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Sikonge, Pascal Ngunda amesema mradi huo umetekelezwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na umekamilika kwa asilimia 100 na umegharimu Sh milioni 297.

    Fedha za mradi huu zimetolewa na Benki ya Dunia kupitia Mpango wa Maendeleo ya Maji Vijijini (WSDP).

    Mradi huo umesaidia kumaliza kero ya maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako