• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sulley Muntari apigwa marufuku kucheza mechi moja

  (GMT+08:00) 2017-05-04 08:57:51

  Kiungo wa kati wa Pascara Sulley Muntari, amepigwa marufuku kucheza mechi moja baada ya kulalamikia matamshi ya kibaguzi.

  Alipewa kadi ya manjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi siku ya Jumapili dhidi ya Cagliari akisema kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi. Mchezaji huyo wa zamani wa Ghana mweye umri wa miaka 32, baadaye aliondoka uwanjani hatua iliyosababisha apewe kadi ya pili ya manjano.

  Mafisa wamesema kuwa sio mashabiki wengi waliofanya ubaguzi kuweza kuchukuliwa hatua.

  Kamati ya nidhamu ilikubaliana kuwa vitendo hivyo vilikuwa vibaya lakini sera zake haziruhusu hatua kuchukuliwa kwa kuwa ni chini ya mashabiki 10 waliohusika.

  Sasa aliyekuwa mshabulijia wa Tottenham Garth Crook anasema kwa kila mchezaji wa kiafrika aliyeheshimiwa katika ligi ya Itaia, anahitaji kugoma wikendi hii iwapo Sulley Mitari hawezi kuondolewa marufuku ya kutocheza mechi moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako