• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza lavunjwa na kutoa nafasi ya kampeni za uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-05-04 10:05:00

    Mchakato wa uchaguzi mkuu wa Uingereza umeanza rasmi baada ya bunge la nchi hiyo kuvunjwa jana.

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May wa Uingereza amekutana na malkia Elizabeth wa pili, ikiwa ni mara yake ya mwisho kukutana na malkia wa Uingereza kama waziri mkuu wa nchi hiyo.

    Bi. Theresa May amesema viongozi wa Umoja wa Ulaya wameitisha Uingereza na kujaribu kuingilia uchaguzi mkuu ujao. Amesisitiza kuwa Waingereza wanapaswa kushikamana na kupata mafanikio katika mazungumzo na Umoja wa Ulaya ili kuijenga nchi yao iwe na nguvu na usalama zaidi.

    Habari zinasema, kwa mujibu wa sheria ya Uingereza, baada ya bunge kuvunjwa, viti vya baraza la makabwela vitakuwa wazi, lakini mawaziri wote wa serikali akiwemo waziri mkuu wataendelea na nyadhifa zao hadi baraza jipya litakapoundwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako