• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtu mwenye silaha asiyejulikana amuua waziri wa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-05-04 10:32:53

    Polisi na serikali ya Somalia wameesema jambazi asiyejulikana amemuua waziri wa masuala ya jamii, kazi na ujenzi wa Somalia Bw Abbas Abdullahi Sheukh jana usiku mjini Mogadishu.

    Waizri wa habari na mwongozo wa taifa wa Somalia Bw Abdurahman Omar Osman amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwenzake aliyeuawa karibu na ikulu ya Somalia, na uchunguzi kuhusu tukio hilo umeanza.

    Bw Osman amesema maofisa wa usalama wameanza uchunguzi na kutafuta chanzo cha mauaji hayo, ambayo yamezusha hofu kwa maofisa wa serikali ya Somalia.

    Polisi mwandamizi amesema kuwa askari wanne wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako